Isaiah 5:1-2

Wimbo Wa Shamba La Mizabibu


1 aNitaimba wimbo kwa ajili ya mmoja nimpendaye,
kuhusu shamba lake la mizabibu:
Mpendwa wangu alikuwa na shamba la mizabibu
kwenye kilima chenye rutuba.

2 bAlililima na kuondoa mawe
na akaliotesha mizabibu bora sana.
Akajenga mnara wa ulinzi ndani yake,
na kutengeneza shinikizo la kukamulia divai pia.
Kisha akatazamia kupata mazao ya zabibu nzuri,
lakini lilizaa matunda mabaya tu.

Copyright information for SwhKC